.

Tuesday, September 7, 2010

SIKILIZA.....SUNDAY SOUL @ EAR KILA JUMAPILI!


SIKILIZA EAST AFRICA RADIO KILA JUMAPILI SAA 10 - 12 JIONI KWA NGOMA KALI ZA LONG TIME KAMA SHOULD I SAY YES,NIGHT SHIFT,LET'S GO DANCING,ELLUSION NK NA DJ 45 KING...WAY BACK HITS!

Monday, September 6, 2010

MPANGO MZIMA.....IIISSSSTAAAAFFFIIIKAAAA TTTTTTVVVV!


Lile ting'a kali no 1 si ndo' limerudi tena babu....kila siku za Jumatatu na Alhamisi mida ya saa 3 usiku usikose kukodolea mimacho runinga yako Live!!!!


WAKALI CHRIS BROWN NA T.I NDANI YA MOVIE MPYA

Wana toka kwa Obama,Chris Brown na T.I wamepata shavu kwenye movie mpya ya TAKERS ambayo imedondoka kitaani tangu Agosti 27 2010

......Sasa Mpango Mzima si ndo' huo sasa au hii tuite Mtoni Movie kwetu si tunaita Bongo Movie au!!!

TIP TOP KUDONDOSHA ALBUM MPYA IDD!

Rais wa Manzese,Madee ataliongoza baraza lake la wasanii siku ya Idd pande za Club San-Siro maeneo ya Sinza kwenye uzinduzi wa album mpya ya kundi BADO TUNAPANDA.

Wana watasindikizwa na vichwa vikali kama Godzilla,Jahfaray,Mwasiti,Lina,Young D na Roma.

Sunday, August 22, 2010

KIDEO CHA LINEX KINAGONGWA LEO..!!

Ni jamaa ambaye amelalamika sana kuhusu mama watoto wake anafahamika kwa jina la Mama Halima kuwa amemtenda sana na hakutegemea hilo kwa bi shosti huyo.

Mchiz anaitwa Linex ambaye ngoma yake ya Mama Halima inafanya vzr sana kwa sasa kwenye Radio station nyingi za hapa bongo.

Sasa mpango mzima ni kuwa kideo cha ngoma hiyo kinachapwa leo na mtu mzima JOHN KALLAGE na siku si nyingi kitaanza kuwa hewani kupitia EATV..

Thursday, August 12, 2010

SSSHHHH... KIJANA ACHA KULALAMIKA TUMIA KURA YAKO..!!


Telavisheni ya Afrika Mashariki (EATV) na East Afrika Radio kwa pamoja zimezinduwa kampeni ya kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifua katika zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jijini Dar es salaam, kampeni hiyo ilizinduliwa katika kipindi cha 5 connect kilicho rushwa moja kwa moja kuanzia saa moja usiku na kuhudhuriwa na wageni vijana pamoja na mjumbe kutoka Tume ya Uchaguzi.

Kituo cha EATV ambacho ndio kituo namba moja kwa vijana na kimechukuwa jukumu hilo kuwahamasisha vijana kutumia kura yao, kutokana na utafiti uliofanywa na kituo hicho kuonyesha kuwa vijana wengi hawashiriki katika kupiga kura.

Katika kufanikisha hilo vituo vya EATV & EAR vitakuwa vinatumia ujumbe wa 'KIJANA ACHA KULALA MIKA TUMIA KURA YAKO' na ujumbe huo utakuwa ukirushwa hewani kupitia televisheni ya EATV na East Afrika Radio.

Ujumbe huu unalengo la kuhakikisha kijana anachaguwa kiongozi bora badala ya kuwaachia wengine shughuli ya kuchaguwa viongozi na badala yake kuishia kulalamika pindi wanapoona uamuzi mbali mbali wa viongozi unawaathiri.

Kampeni hii ambayo tumetumia picha za video na sauti za vijana mbalimbali itaendelea hadi Oktoba 30 na vile vile ifikapo septemba tutazinduwa kipindi maalum kwa ajili ya uchaguzi kiitwacho UCHAGUZI XPRESS LIVE.

Kipindi hicho tutajadili mada mbalimbali zenye lengo la kumjenga kijana ufahamu kuhusiana na umuhimu wa yeye kushiriki katika uchaguzi mkuu ili waweze kuchaguwa viongozi bora na wenye sifa.

Friday, August 6, 2010

WANA WEEKEND NJEMA...ILA GAMBE KIAINA AU VP!!!!

MWANA KUGOMBEA U-PREZIDAA!

Wyclef Jean mwana toka Haiti ametangaza nia ya kugombea urais wa Haiti utakaofanyika mwezi November tarehe 28 mwaka huu...Kila la heri!

Tuesday, August 3, 2010

WATENGWA WAMKUMBUKA FAZA NELLY!

RIP NELSON CHRIZOSTOM BUCHARD AKA FAZA NELLY (1976-2006)

Kundi la Watengwa toka A-Town chini ya JCB wametoa audio na video ya kumkumbuka mwanaharakati na memba wa X-Plastaz,Faza Nelly ambaye alifariki 29 March 2006 kwa kuchomwa kisu Mkoani Arusha iitwayo "SITOWASAHAU MILELE"

Ndani ya ngoma hiyo pia wamekumbukwa wanaharakati kibao wa muziki wa Tanzania (REST IN PEACE..BROS & SISTAZ)

Tuesday, July 27, 2010